Download presentation
Presentation is loading. Please wait.
Published byDjaja Setiabudi Modified over 6 years ago
1
WAJIBU WA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KATIKA URATIBU WA NGOs
MKUTANO WA 13 wa WATAALAM WA MAENDELEO YA JAMII 26 – 29 Novemba, 2018 Hoteli ya lush garden - arusha
2
1.0 MALENGO YA WARSHA Kuwezesha uelewa wa Sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kuwezesha uelewa wa majukumu ya Maafisa Maendeleo ya Jamii katika uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kuwezesha uelewa wa taratibu za usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kuwezesha uelewa wa ufuatiliaji wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kuwezesha uelewa wa pamoja juu ya maboresho katika Usimamizi wa mashirika yasiyo ya Kiserikali Nchini.
3
2.0 TAFSIRI YA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI
Kwa mujibu wa Sera na Sheria ya NGOs; Kikundi cha hiari cha watu au mashirika Kilicho huru Kisicho cha kidini wala kisiasa Kisicho cha kugawana faida Kiwe kwa ajili ya kuhudumia jamii na si wanachama wake
4
3.0 VYANZO VYA SHERIA KWA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania/1977 Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali/2001 Sheria ya NGOs, Na.24/2002 (kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005) Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
5
4.0 MAPITIO YA KANUNI ZA SHERIA YA NGOS
Serikali imefanya mapitio ya Kanuni ya NGOs Na. 152/2004 ili iendane na wakati na kuweka uwazi na uwajibikaji wa Asasi hizo. Marekebisho ya Kanuni yamekamilika na kutangazwa kwenye gazeti la Seriakli Na. 609 la tarehe 19/10/2018 yanajulikana kama NGOs Ammendment Regulation,2018 Marekebisho yamefanyika kwa kuongeza sehemu ya Nne ambayo inazungumzia Uwazi na Uwajibikaji katika Masuala ya Fedha.
6
4.1 MAUDHUI YA KANUNI ZILIZOREKEBISHWA
Kuweka utaratibu unaozitaka NGOs kuweka wazi vyanzo vya rasilimali zinzoendesha miradi yao, matumizi yake na shughuli zinazotekelezwa s.12 Kuzitaka NGOs kutangaza kupitia vyombo muhimu vya mawasiliano katika jamii mikataba ya ufadhili unaozidi milioni 20. Regulation.13 Kusimika misingi ya uwazi na uwajibikaji kifedha ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi mabaya ya fedha za ufadhili zinazotolewa. Regulation 14
7
Maudhui… Kuweka uataratibu wa NGOs kuwajibika kwa wananchi wanaowahudumia kupitia mifumo ya Serikali za mitaa iliyopo. Regulation 15 Kanuni hizi pia zimeboresha majedwali yatakayotumika kupokea taarifa mbalimbali
8
Manufaa ya marekebisho yaliyofanyika
Kujenga misingi ya uwazi na uwajibikaji kifedha Serikali kuweza kufahamu mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maendeleo Kushirikiana na mamlaka za Serikali za mitaa kupitia Wasajili Wasaidizi katika uratibu, usimamizi na utoaji taarifa za miradi ya maendeleo inayoendeshwa na NGOs Kuiwezesha Serikali kupitia Wizara ya Fedha kuweka kumbukumbu ya fedha za wafadhili zinaingia nchini kupitia NGO
9
Manufaa ya marekebisho
Kuijengea uwezo jamii kufahamu miradi inayotekelezwa na NGOs katika maeneo yao na kuhoji utekelezaji wa miradi hiyo Kujenga mifumo ya pamoja ya kisheria katika kulinda rasilimali fedha Kuwezesha uboreshaji wa taarifa kwenye kanzi data ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi mbalimbali
10
5.0 WAJIBU WA CDOs KATIKA URATIBU WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Msingi wa Kisheria kwa CDOs kuratibu Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ---- S.22(1) “The Registrar shall, for the purpose of facilitating registration ………. appoint a public officer amongst public officers within the region or district”
11
5.0 MAJUKUMU YA CDOs Kuwezesha usajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kufuatilia shughuli zinazotekelezwa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuhakikisha kama zinanufaisha jamii Kuandaa taarifa kuhusu NGOs na kuwasilisha kwa Msajili wa NGOs kila mwaka Kuratibu uwasilishaji wa mipango kazi ya NGOs na kuingiza katika mipango ya wilaya/ mkoa husika
12
MAJUKUMU YA CDOs ……. Kutatua migogoro inayoibuka katika Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kuwezesha utekelezaji wa Sera na Sheria ya NGOs Kuwezesha na kukuza ushirikiano kati ya NGOs na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo Kusimamia uanzishaji wa kamati za maadili za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika ngazi husika
13
MAJUKUMU YA CDOs……. Kusimamia chaguzi za viongozi wa Baraza la Taifa la NGOs katika ngazi husika Kuhamasisha uanzishaji wa mitandao ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika maeneo husika ili kuimarisha ushirikiano miongoni mwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
14
6.0 MSINGI WA URATIBU WA NGOs
Kutambua Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Kubaini michango ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa maendeleo ya jamii/taifa Kudhibiti vitendo vyenye nia ovu vinavyoweza kutekelezwa na NGOs au kupitia NGOs
15
7.0 TARATIBU ZA USAJILI WA NGOs
Kifungu cha 12(1) – Maombi yanawasilishwa kwa Msajili kupitia fomu maalumu (NGO A Fomu Na.1) Viambatisho vya usajili – Kifungu cha 12 (2) 1.Katiba (nakala 3 zilizojaladiwa) 2.Muhtasari wa kikao cha wanachama 3.Wasifu (CV) wa viongozi na 4.Fomu ya maombi (NGO A Fomu Na.1) + S/Duty 5.Barua ya utambulisho kutoka kwa DCDO/RCDO
16
8.0 UFUATILIAJI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI
Kutembelea na kukagua utendaji kazi wa NGOs Taarifa za kazi Kupitia kamati za maadili na mitandao ya NGOs katika ngazi husika
17
9.0 UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA NGOs
Wasajili Wasaidizi wanao wajibu wa kuhakikisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya uwazi na uwajibikaji. Misingi ya uwazi na uwajibikaji inasisitizwa kwenye Sera ya Taifa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2001, Sheria ya NGOs No.24/2002 na kanuni zake. Misingi ya Uwazi na uwajibikaji imejikita katika maeneo makuu manne yafuatayo; Uwajibika wa juu (upward accountability) Uwajibikaji wa chini (Downward accountability)
18
UWAZI NA UWAJIBIKAJI wa nje (External Accountability) Uwajibikaji wa ndani (Internal Accountability)
19
10.0 HITIMISHO Kwa kuhitimisha naomba kutoa maelekezo yafuatayo: Wajibu wa Maafisa Maendeleo ya Jamii kwenye kusaidia usajili na usimamizi wa NGOs ni mtambuka, na kwa kua suala la usajili na usimamizi ni la kisheria hivyo ni vyema watekeleze majukumu hayo kwa mujibu wa Sheria na mingozo iliyopo. Sheria ya NGOs kama Sheria ya Nchi inasomeka na Sheria nyingine na hivyo haki na wajibu wa NGOs visimamiwe kikamilifu kwa kufuata taratibu. Ni vyema tuzingatie na kuhakikisha kuwa Mikataba yote ya NGOs na wafadhili inasimamia maslahi ya umma
Similar presentations
© 2025 SlidePlayer.com Inc.
All rights reserved.