Download presentation
Presentation is loading. Please wait.
1
HPV na SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
MTAALA WA UICC WA HPV na SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
2
Slaidi Sura ya 7 Utunzaji wa kupunguza maumivu wa saratani ya mlango wa kizazi Anne Merriman, MD Mwasisi na Mkurugenzi wa Sera na Programu za Kimataifa, Hospice Africa, Uganda Rose Kiwanuka, RN Mratibu wa Nchi, Chama cha Utunzaji wa Kupunguza Maumivu cha Uganda Eduardo Rosenblatt, MD Mkuu wa Kitengo, Kitengo cha Biolojia ya Mnururisho Tumizi na Tibaredio, Sekta ya Afya ya Binadamu, IAEA Gillian Fyles, MD Kiongozi wa Kimatibabu, Programu ya Usimamizi wa Maumivu na Dalili/Utunzaji wa Kupunguza Maumivu BCCA - Kituo cha Kusini cha Ndani, Kanada Megan O’Brien, PhD Mkurugenzi, Mpango wa Mfiko wa Kimataifa wa Kutuliza Maumivu (GAPRI), UICC Maria Stella de Sabata, MA Mkuu wa Programu, UICC 01 Sura hii itazungumzia utunzaji wa kupunguza maumivu kwa saratani ya mlango wa kizazi.
3
02 Yaliyomo Slaidi Sura hii inajumuisha
1. Mtazamo wa utunzaji wa kupunguza maumivu 2. Udhibiti wa maumivu. 3. Mnururisho na tibakemikali ya kupunguza maumivu 4. Matibabu ya dalili za kawaida katika saratani ya mlango wa kizazi 5. Matibabu yanayotumika zaidi kwa kawaida
4
1. Mtazamo wa utunzaji wa kupunguza maumivu
Slaidi 03 1. Mtazamo wa utunzaji wa kupunguza maumivu Karibu katika ulimwengu wa utunzaji wa kupunguza maumivu. Maadili yetu yanahakikisha ukarimu kwa hivyo tafadhali ingia, jihisi kuwa nyumbani na pata kujua jinsi wewe pia unaweza kusaidia wale ambao wanateseka sana bila msaada katika nchi nyingi zinazoendelea.
5
04 Utunzaji wa kupunguza maumivu Slaidi
Utunzaji wa kupunguza maumivu ni mtazamo ambao unaboresha hali ya maisha ya wagonjwa na familia zao ambazo zinakumbana na matatizo yanayohusiana na magonjwa yanayotishia maisha, kupitia: uzuiaji na utulizaji wa maumivu kwa njia za Utambulisho wa mapema na utathmini na utibabu maasumu wa maumivu na matatizo mengine, ya kimwili, kisaikolojia na kijamii na pia kiroho Source: WHO 2002 Kwa mujibu wa ufafanuzi wa Shirika la Afya Duniani, utunzaji wa kupunguza maumivu ni mtazamo ambao unaboresha hali ya maisha ya wagonjwa na familia zao ambazo zinakumbana na matatizo yanayohusiana na magonjwa yanayotishia maisha, kupitia kwa uzuiaji na utulizaji wa mateso kwa njia za utambulisho wa mapema na utathmini na utibabu maasumu wa maumivu na matatizo mengine, ya kimwili, kisaikolojia na kijamii na pia kiroho. Utunzaji wa kupunguza maumivu ni kamilifu katika mtazamo wake kwa vile unajumuisha maumivu pamoja na vilevile matatizo mengine ya kimwili, kisaikolojia na kijamii na pia kiroho.
6
05 Mwendeleo wa utunzaji wa kupunguza maumivu Barani Afrika Slaidi
Hii nii tafsiri maarufu ya kimchoro inayoonyesha kuwa utunzaji wa kupunguza maumivu kwa saratani au ugonjwa unaotishia maisha unafaa kuanzishwa kutoka wakati wa ubainishaji wa ugonjwa na kuendelea hadi kifo. Baada ya kifo cha mgonjwa, timu ya utunzaji wa kupunguza maumivu husaidia familia iliyofiwa katika kipindi cha msiba. Hata hivyo, tafsiri hii hufaa nchi zilizoendelea, pale ambapo matibabu ya kushughulikia ugonjwa yanapatikana kwa wote. Barani Afrika kwa mfano, chini ya asilimia 5 ya watu wana uwezo wa kufikia utunzaji kama huu, na kwa hivyo sehemu inayoonyesha eneo hili imesongeshwa juu ili kuonyesha uchache wa matibabu kama haya na mahitaji makubwa zaidi ya utunzaji wa kupunguza maumivu ili kufikia hata wale ambao hawajawahi kumwona mfanyakazi wa huduma za afya.
7
06 Timu ya utunzaji wa kupunguza maumivu Slaidi
Utunzaji wa kupunguza maumivu unahitaji timu iliyo na utaalamu mbalimbali. Katika nchi zilizoendelea timu hii hujumuisha: Mwuguzi Daktari Mtaalamu wa tibamaungo Mtaalamu wa huduma za kazi Mfanyakazi wa huduma za kijamii Mshauri wa kiroho … Katika nchi zinazoendelea huenda ikawa ni mtu mmoja: mwuguzi aliye na utaalamu mbalimbali mwenyewe Utunzaji wa kupunguza maumivu ni kamilifu pia kwenye timu. Katika nchi zilizoendelea timu huwa na utaalamu mbalimbal, wakiwemo madaktari, wauguzi, wafanyakazi wa huduma za kijamii, wataalamu wa tibamaungo, wataalamu wa huduma za kazi, washauri wa kiroho na wengineo. Katika nchi zinazoendelea timu hii mara nyingi inaye tu mwuguzi wa utunzaji wa kupunguza maumivu. Kwa hivyo, mafunzo ya mwuguzi wa utunzaji wa kupunguza maumivu yanahitaji kutilia maanani sehemu hizi zote. Mwuguzi ni lazima awe yote kwa yote kwa mgonjwa katika hali tofauti sana zinazotokana na imani za kitamaduni na ufukara. Ni hali ya kusikitisha sana-lakini utunzaji wa kupunguza maumivu unaweza kubadilisha sura ya kifo kwa wagonjwa ikiwa utaweza kutolewa kwa njia ambayo inafaa kwa utamaduni wa mahali na rasilimali zinazopatikana. Barani Afrika, utunzaji wa kupunguza maumivu unapatikana sasa katika nchi 14, ingawa mara nyingi huwa haufikii idadi yote ya watu.
8
07 Utunzaji wa kupunguza maumivu, huduma ya msaada ,
Slaidi Utunzaji wa kupunguza maumivu, huduma ya msaada , udhibiti wa maumivu 07 Huenda ufafanuzi ukawa wa kuleta utata. Dawa na utunzaji wa kupunguza maumivu ni LAZIMA ujumuishe: Huduma ya msaada NA Udhibiti wa maumivu Udhibiti wa maumivu na dalili ni muhimu sana katika utunzaji wa kupunguza maumivu. Maumivu makali hayaruhusu utunzaji kamilifu kwani wagonjwa na familia huwa wamesononeka kwa kiasi kuwa hawawezi kufikiria, kupanga, au kuomba. Tangu mwaka wa 1990, Barani Afrika, mofini ya kumeza ya bei nafuu - ambayo inaweza kutumiwa nyumbani na mgonjwa - inapatikana katika nchi 14 kati ya 56 za Bara hili, na inafikia tu sehemu ndogo ya idadi ya watu.
9
08 Hospisi na utunzaji wa kupunguza maumivu (1) Slaidi
Hospisi si jengo. Ni falsafa ya utunzaji inayoashiria “ukarimu” Mgonjwa ni mgeni na anafaa kuwa na chaguo katika maswala yote, yakiwemo matibabu, hadi kifo Mgonjwa ndiye kiini cha utunzaji na cha timu. Utunzaji unaotolewa na timu unafaa kujumuisha: Mawasiliano ya kawaida na mgonjwa Utoaji wa taarifa kuhusu ubainishaji wa ugonjwa, ubashiri wa ugonjwa, matibabu nachaguo za utunzaji Msaada wa kihisia na kijamii Msaada wa kiutendaji na kifedha Kuhakikisha mwendelezo ya utunzaji Kuchunguza na kutoa mwitikio kwa mahitaji maalum Dhana ya hospisi ni mabadiliko kutoka kwa mazingira ya hospitali, ambapo wagonjwa ni “wazuri” ikiwa wanafanya wanavyoambiwa au ni “wasiopendwa” ikiwa wanapinga matumizi ya dawa au matibabu. Katika hospisi, mgonjwa ni mgeni na ana chaguo katika mambo yote hadi kifo. Hiki ni kiungo muhimu cha utunzaji wa kupunguza maumivu na watoa huduma waliopewa mafunzo na walio na njia nzuri za kuwasiliana. Utunzaji unaotolewa na timu ya matibabu kwa wagonjwa walio na saratani iliyoendelea unafaa kujumuisha: mawasiliano ya kawaida na mgonjwa, utoaji wa taarifa (kuhusu ubainishaji wa ugonjwa, ubashiri wa ugonjwa, matibabu na chaguo za utunzaji) na msaada (wa kihisia, kijamii, kiutendaji na kifedha) kuhakikisha mwendelezo wa utunzaji, na kuchunguza na kutoa mwitikio kwa mahitaji maalumu.
10
09 Hospisi na utunzaji wa kupunguza maumivu (2) Slaidi
Istilahi “utunzaji wa kupunguza maumivu” (palliative care) ilikuzwa nchini Kanada na Prof. Balfour Mount, kwa vile “hospisi” ilikuwa imekuwa sawa na “nyumba ya kifo”. “Palliative” hutokana na neno la Kilatino “pallium” ambalo humaanisha joho au blanketi Neno la Kilatino “pallium” liliashiria aina ya joho katika Ugiriki na Urumi za Kale. Neno “pallium” lilibadilishwa kuunda “palliate,” kivumishi kinachomaanisha “funikwa” au “fichwa” na kitenzi kinachomaanisha “kufunika,” “ kuvalisha, au “kuhifadhi.” Leo ”palliation” huashiria kuficha au kufunika ubaya au uovu na hupendekeza maana ya kupunguzwa kwa athari mbaya za uovu au ugonjwa.
11
Slaidi Utunzaji wa kupunguza maumivu: jinsi ulivyotambulika - mifano kadhaa 10 1987: Chuo cha Madaktari cha Royal (London) kilitangaza Dawa ya Kupunguza Maumivu kuwa taaluma 1993: Utunzaji wa Kupunguza Maumivu ulifunzwa kwa wanafunzi wa utibabu wa shahada ya kwanza na wauguzi nchini Uganda na kujumuishwa kwenye mtaala wa utibabu na uuguzi mnamo mwaka wa 2004 2007: Vyuo nchini Marekani vilitambua Utunzaji wa kupunguza maumivu kama taaluma Miaka ishirini baada ya Dame Cicely Saunders, mwasisi wa harakati ya kisasa ya Hospisi, alifungua Hospisi ya St Christopher’s jijini London, vyuo vya Royal Collleges nchini Uingereza vilitambua Utunzaji wa Kupunguza Maumivu kama taaluma. Ilichukuwa miaka mingine 20 kwa Kamati za Marekani kutambua taaluma hiyo. Ni muhimu kwa taaluma hii kutambuliwa na kuheshimiwa na wafanyakazi wenza Barani Afrika na kwingineko ili waweze kuwaelekeza wagonjwa walio na mahitaji, kujifunza mambo muhimu na kutambua kwamba utunzaji hauishii kwenye mlango wa hospitali. Hatimaye wafanyakazi wote wa kiafya wanaweza kutoa utunzaji na kuwaelekeza wagonjwa ili utunzaji wa kupunguza maumivu uweze kuwafuata wagonjwa hadi nyumbani kwao.
12
11 “K” tano kuhusu utunzaji wa kupunguza maumivu Slaidi Kukadiria
Kadiria hali ya mgonjwa na tambua mahitaji yake ya kimatibabu. Kadiria ufahamu, mahangaika na ujuzi wa mgonjwa jinsi unavyohusiana na ugonjwa na matibabu yake. Kushauri Fafanua jinsi ya kuzuia na kudhibiti dalili, na funza mbinu za ujuzi zinazohitajika , idadi ndogo kwa wakati mmoja, kwa kuonyesha na kutazama utekelezaji. Kukubali Baada ya kutoa taarifa na kufunza mbinu za ujuzi, hakikisha kuwa mgonjwa anajua ni kipi cha kufanya na kwamba anataka kukifanya. Mpe uwezo wa kuchukua dhima. Mpe mgonjwa msaada katika kujisimamia mwenyewe na katika utunzaji wa familia. Kusaidia Hakikisha kwamba mgonjwa na familia yake wana ruzuku ya kutosha ili kukabiliana na hali ngumu na toa huduma inayohitajika. Toa maagizo yaliyoandikwa kama kumbusho la kile kinachohitajika kufanywa, zikiwemo picha ikiwa zitahitajika kwa wale ambao hawawezi kusoma. Kupanga Ratibu muda wa ziara inayofuata. Hakikisha kuwa mgonjwa, familia yake na watoa huduma wengine wanajua mahala pa kwenda ikiwa wana maswali au mahangaiko. Shirika la Afya Duniani linaonyesha “K” tano za utunzaji wa kupunguza maumivu: Kukadiria, Kushauri, Kukubali, Kusaidia na Kupanga. Marejeleo: WHO, Udhibiti Jumlishi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi, 2006
13
Slaidi 12 2. Udhibiti wa maumivu
14
Slaidi Udhibiti wa maumivu kwa wanawake walio na saratani ya mlango wa kizazi (1) 13 Maumivu ni dalili ya kawaida kwa wanawake wengi walio na saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea Kwa kutumia udhibiti unaofaa, maumivu ya saratani yanaweza kupunguzwa kwa takriban asilimia 90 ya wagonjwa Dawa za kupunguza maumivu zinazoitwa Opioid analgesics ni kiungo muhimu sana cha matibabu ya maumivu ya saratani Matibabu ya maumivu hayafai kuachwa hadi wakati wa hatua za mwisho za ugonjwa, ila, yanafaa kujumuishwa katika matibabu ya hatua zote inavyohitajika Huku saratani ya mlango wa kizazi ikiweza kutibiwa katika nchi zilizoendelea, katika nchi nyingi zinazoendelea huu ndio ugonjwa unaoongoza katika kusababisha vifo vya wanawake. Ufahamu kuhusu saratani ya mlango wa kizazi ni mchache. Ugunduzi na matibabu ya mapema ni nadra. Chanjo kwa wasichana ndio sasa zinaanza kutumika, na, zinapotekelezwa kwa utaratibu uliopangwa vizuri, matokeo yake hayatatambulika kwa miaka mingi ijayo. Tibaredio ni nadra au haipo katika nchi zinazoendelea. Nchini Uganda, kwa mfano, kuna kituo kimoja cha tibaredio na onkolojia kwa watu wapatao millioni 33, na theluthi moja ya nchi za Kiafrika hazina huduma yoyote ya saratani. Umaskini hauwaruhusu wanawake kusafiri ili kutafuta msaada wa kimatibabu, na hata kama wangeweza kuugharimia usafiri, hawawezi kudumisha mahitaji yao kwenye jiji lililo mbali kutoka nyumbani. Kwa hivyo, wanawake wanajiwasilisha wakiwa wamechelewa, hivyi kwamba mara nyingi suluhisho pekee lililobaki kwa mateso yao makuu ni utunzaji wa kupunguza maumivu. Wanawake wanakufa huku wakiwa na maumivu makali ya kimwili na kisaikolojia, wakati mwingine wakiwa wameachwa na waume wao kwa sababu ya miiko ya kitamaduni na kuacha nyuma familia changa. Hata hivyo, kwa udhibiti wa kutosha, maumivu ya saratani yanaweza kupunguzwa kwa takriban asilimia 90 ya wagonjwa.
15
Slaidi Udhibiti wa maumivu kwa wanawake walio na saratani ya mlango wa kizazi (2) 14 Dalili zingine zinaweza pia kutokea katika saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea, kutokana na saratani yenyewe na athari zake au wakati mwingine kutokana na athari za dawa Kama ilivyo katika maumivu, nyingi za dalili hizi zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia hatua rahisi Kuna pande zingine zinazohusiana na mateso zaidi ya zile za kimwili Dalili zingine zinaweza pia kutokea katika saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea, kutokana na saratani yenyewe na athari zake au wakati mwingine kutokana na atharii za dawa. Kama iliyvo katika maumivu, nyingi za dalili hizi zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia hatua rahisi. Kuna pande zingine zinazohusiana na mateso zaidi ya zile za kimwili, jinsi inavyoonekana katika slaidi ifuatayo.
16
15 Jumla ya Mateso: Woodruff Jumla ya Mateso Maumivu Kiroho Kitamaduni
Slaidi Jumla ya Mateso: Woodruff 15 Jumla ya Mateso Maumivu Kijamii & kifedha Kiroho Kitamaduni Kisaikolojia Dalili za Kimwili Sisi ni viumbe changamani wenye hali za kimwili, kisaikolojia na kijamii na pia kiroho. Mateso yanaweza kutokea katika mojawapo ya maeneo haya, na yote yanafaa kutiliwa maanani wakati wa kukadiria mgonjwa aliye na maumivu. Dr. Cicely Saunders aliyaita haya “Jumla ya Maumivu”.
17
16 Uainishaji wa maumivu Visera (Visceral) Neuropathia (Neuropathic)
Slaidi Uainishaji wa maumivu 16 Msisimuo wa neva (Nociceptive) Somatiki (Somatic) Visera (Visceral) Mseto (Mixed) Neuropathia (Neuropathic) Ni muhimu kuweza kuainisha maumivu ambayo mgonjwa anayapitia kwa vile hii itaweza kukuelekeza kwa matibabu saidizi yanayofaa yaani ikiwa kuna maumivu ya kineuropathia dhukuru kuongeza amitriptyline au gabapentin; katika hali ya maumivu ya visera dhukuru kuongeza steroidi. Ufafanuzi Maumivu yanayotokana na msisimuo wa neva (nociceptive): yanasababishwa na kusisimuliwa kwa nyuzi za neva za pembeni ambazo huitikia tu kiamshi kinachokaribia au kinachozidi kiwango haribifu Maumivu ya kisomatiki (somatic) : huanzia kwenye ngozi (somatiki ya juu juu) na kwenye tishu za ndani (somatiki ya kina) Maumivu ya visera (visceral): huanzia kwenye visera (viungo) Maumivu ya kineuropathia (neuropathic): husababishwa na uharibifu au ugonjwa unaoathiri sehemu ya katikati au ya pembeni ya mfumo wa neva ambayo huhusika katika hisia za mwili.
18
17 Udhibiti wa maumivu Slaidi Udhibiti unaofaa kwa maumivi huhusisha:
Ufuatiliaji wa karibu wa dalili Matibabu ya mapema na ya hima ya kutumia vituliza maumivu - Huduma ya msaada iliyotiliwa maanani Matibabu ya kuweka ganzi au ya kupunguza machungu (neuroablative) katika visa teule (kuwaelekeza wagonjwa walio na maumivu yasiyodhibitika kwa urahisi hadi kwenye zahanati zilizo na utaalamu mbalimbali wa kudhibiti maumivu) Udhibiti unaofaa kwa maumivu huhusisha: Ufuatiliaji wa karibu wa dalili Matibabu ya mapema na ya hima ya kutumia vituliza maumivu Huduma ya msaada iliyotiliwa maanani Matibabu ya kuweka ganzi au ya kupunguza machungu (neuroablative) katika visa teule
19
18 Ni nini cha Kujumuishwa katika Usimamizi wa Maumivu: MUJEMMUM
Slaidi Ni nini cha Kujumuishwa katika Usimamizi wa Maumivu: MUJEMMUM 18 Mwanzo (Onset) Yalianza lini? Yanadumu kwa muda gani? Yanatokea mara ngapi? Usababishaji/Upunguzaji wa Maumivu (Provoking/Palliating) Yanaanzishwa na nini? Yanapunguzwa/kinayazidishwa na nini? Jinsi (Quality) Yanaleta hisia zipi? Eneo/ Usambaaji (Region/Radiation) Yako wapi? Je yanasambaa popote? Makali (Severity) Dalili hii ina makali ya kiwango kipi? Sasa hivi? Katika hali nzuri zaidi? Katika hali mbaya zaidi? Kwa wastani? Dalili zozote nyingine ambazo zinaandamana na dalili hii? Matibabu (Treatment) Ni dawa zipi na matibabu yapi unayoyatumia kwa sasa? Yana ufanisi upi? Yanayo athari zozote? Ni dawa zipi na matibabu yapi umeyatumia katika wakati uliopita?) Ufahamu/ athari kwako (Understanding/impact on you) Unaamini nini kinachosababisha dalili hii? Dalili hii inakuathiri vipi wewe na/au familia yako? Maadili (Values) Lengo lako la kufarijika au la kiwango kinachokubalika katika dalili hii ni lipi? Kunayo maoni au hisia zingine zozote kuhusu dalili hii ambazo ni muhimu kwako au kwa familia yako? Slaidi hii ni kisaidizi cha kumbukumbu chenye manufaa (MUJEMMUM au OPQRSTUV kwa maneno ya kimombo) wakati wa kukadiria maumivu. Hakikisha kuwa umetilia vipengele hivi vyote maanani ili kupata taswira kamili ya maumivu ya mgonjwa.
20
maumivu yasiyovumilika
Slaidi Mifano ya viwango vya maumivu: 19 1) 2) 3) Hakuna maumivu kidogo wastani mbaya sana kali zaidi maumivu yasiyovumilika Mifano michache ya viwango vya maumivu imewasilishwa katika slaidi hii. Watu walio na maumivu huenda wasiweze kueleza mitazamo yao ya maumivu, na viwango vya maumivu vinaweza kuwa zana yenye manufaa katika kukadiria makali ya maumivu. hayaumizi yanaumiza kidogo yanaumiza zaidi yanaumiza hata zaidi yanaumiza kabisa yanaumiza vibaya
21
20 Udhibiti wa maumivu Slaidi Udhibiti wa maumivu unaweza kujumuisha:
Tiba ya kifamakalojia: matumizi ya ngazi ya Kutuliza Maumivu ya WHO ni zana muhimu sana Tiba nyingine zinapofaa: tibaredio tibakemikali upasuaji Tiba za kutimiza zinazotumika kama viongezo Kuchukua mtazamo wa utaalamu mbalimbali katika usimamizi wa maumivu kunahimizwa. Udhibiti wa maumivu unaweza kujumuisha: tiba ya kifamakolojia, tiba nyingine zinapofaa (tibaredio, tibakemikali, upasuaji), tiba za kutimiza zinazotumika kama viongezo. Kuchukua mtazamo wa utaalamu mbalimbali kunahimizwa.
22
3 2 1 21 Ngazi ya WHO ya utulizaji wa maumivu Slaidi
Madawa ya aina ya afyuni yaitwayo opioidi (opioid) kwa maumivu ya wastani hadi yale makali (mofini) (+/- isiyo opioidi (non-opioid) +/- kisaidizi (adjuvant) 3 Opioidi kwa maumivu ya kiwango cha chini hadi yale ya wastani (kodeini) +/- isiyo opioidi, +/- kisaidizi 2 Shirika la Afya Duniani linapendekeza hatua zifuatazo katika utulizaji wa maumivu: 1- Anza kwa kutumia dawa isiyo ya aina ya opioidi kama vile paracetamol, paracetamol, aspirin au ibuprofen 2- Ikiwa maumivu yataendelea ama kuongezeka, mpatie mgonjwa opioidi kwa maumivu ya kiwango cha chini hadi yale ya wastani, k.m. kodeini pamoja na au bila dawa isiyo aina ya opioidi. Ikiwa mgonjwa ameagiziwa opioidi, hatua kwa hatua, mpatie haluli ili kuzuia uyabisi wa tumbo. Ongeza dawa ya kuzuia kutapika ikiwa inahitajika. 3- Ikiwa maumivu yataendelea au kuongezeka, mpatie mofini, pamoja na au bila ya dawa isiyo aina ya opioidi. Zingatia kuwa katika nchi nyingi, opioidi huhitaji kuagizwa chini ya ushauri na usimamizi wa kitatibabu Isiyo opioidi (paracetamol au ibuprofen) (+/- kisaidizi) 1
23
22 Lengo la udhibiti wa maumivu: Slaidi Kuboresha hali ya maisha
Kupunguza maumivu Kuboresha utendaji Wa kimwili Wa kisaikolojia na kijamii Kupunguza athari mbaya Lengo la udhibiti wa maumivu ni kuweza kuboresha hali ya maisha, kupunguza maumivu, kuboresha utendaji na kupunguza athari mbaya.
24
23 Kanuni za udhibiti wa maumivu: Slaidi
Kadiria kwa undani lakini kwa haraka Patiana vituliza maumivu mara kwa mara Tumia njia ya kinywa kila inapowezekana Fuata mtazamo wa hatua kwa hatua Kumbuka kuruhusu utumiaji wa viwango vya opioidi ambavyo vitasababisha tofauti Tumia dawa saidizi pale zinapodokezwa Tarajia athari Fuatilia mgonjwa Elimisha mgonjwa na familia Tumia mtazamo wa utaalamu mbalimbali Slaidi hii inatoa muhtasarii wa kanuni 10 muhimu zaidi katika udhibiti wa maumivu.
25
24 Dawa za kawaida za maumivu: Slaidi Zisizo opioidi Paracetamol
Ibuprofen Saidizi/ya msaada Amitriptyline Gabapentin Steroidi Opioidi Mofini Dihydrocodeine Dawa za kawaida za maumivu zimeweza kutolewa kwa muhtasarii katika slaidi hii. Istilahi saidizi na ya msaada zina maana sawa na zinaashiria dawa za kifamakolojia ambazo zina matumizi ya kimsingi yaliyo tofauti na maumivu lakini zilizo na nguvu za kutuliza maumivu na ambazo hutumika mara kwa mara katika udhibiti wa maumivu. Zinaweza kutumiwa pekee lakini kwa kawaida hutumiwa pamoja na opioidi ikiwa maumivu ni ya kiwango cha wastani au ni makali.
26
S M W K O 25 Kufanya matibabu ya maumivu kuwa yenye nguvu Slaidi
Saidizi; Dawa saidizi (za msaada) zinafaa kutumiwa kutibu maumivu ya neva (amitriptyline) au maumivu ya mfupa (steroidi) Marekebisho yanafaa kufanywa endapo matibabu hayaendelei kutuliza maumivu. Haya yanaweza kujumuisha kuongeza kipimo cha dawa, kuongeze dawa nyingine, au kubadilisha dawa Mara kwa mara; Kumeza dawa mara kwa mara kuna manufaa zaidi kuliko kumeza dawa za maumivu “inavyohitajika” Wakati wa kulala; Viwango vya dawa zinazomezwa wakati wa kulala vinaweza kuongezwa ili kutuliza maumivu bila kutatiza usingizi Kunyweka; Dawa za njia ya kinywa zina nguvu zina nguvu sawa na zile za sindano, na rahisi zaidi kutumika Slaidi hii inaonyesha kisaidizi kingine cha kumbukumbu chenye manufaa kwa matibabu ya maumivu yenye ufanisi. Okoa; Dawa za kuokoa zinaweza kutolewa endapo maumivu yatarudi kabla ya wakati ufuatao wa kipimo kilichoratibiwa. Hiki ni kipimo sawa na kile kilichoratibiwa na hutolewa kama nyongeza ya kipimo cha kawaida , na wala si badala yake.
27
26 Tiba za maumivu sizisotumia dawa Slaidi
Katika baadhi ya tamaduni, msaada wa kihisia, kugusa kimwili au kukanda, kupiga taswira akilini, kuvuta mawazo, maombi, au tafakuri zinaweza kutumika Hizi hazifai kutumiwa kama mbadala wa dawa za maumivu Wagonjwa wanaweza kutaka kuzitumia kama tiba za kutimiza Katika baadhi ya tamaduni, msaada wa kihisia, kugusa kimwili au kukanda, kupiga taswira akilini, kuvuta mawazo, maombi, au tafakuri huenda zinaweza kutumiwa kama tiba za maumivu zisizotumia dawa. Inafaa kutiliwa maanani kwamba shughuli hizi zote hazifai kutumiwa kama mbadala wa dawa za maumivu; hata hivyo, huenda wagonjwa wakataka kuzitumia kama tiba za kutimiza.
28
27 Mawasiliano kuhusu dawa Slaidi
Toa maelezo kuhusu vipimo vya dawa kwa uangalifu na mruhusu mgonjwa kuuliza maswali Toa maagizo yaliyoandikwa katika lugha ya kimsingi ya mgonjwa Tumia picha au vielelezo vya taswira Toa vielelezo vya kumsaidia mgonjwa kukumbuka maagizo ya kumeza dawa Ni muhimu kuweza kuwasiliana na mgonjwa kwa njia inayoeleweka kuhusu dawa. Hii huhitaji muda wa kujibu maswali, lugha rahisi na pengine matumizi ya vielelezo vya picha.
29
28 Mifano ya vielelezo vya vipimo na masharti ya matumizi ya dawa
Slaidi Mifano ya vielelezo vya vipimo na masharti ya matumizi ya dawa 28 Mifano ya vielelezo saidizi vya vipimo na masharti ya matumizi ya dawa vimeonyeshwa kwenye slaidi hii.
30
3. Mnururisho na tibakemikali ya kupunguza maumivu
Slaidi 29 3. Mnururisho na tibakemikali ya kupunguza maumivu
31
Slaidi Mnururisho wa kupunguza makali kwa wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi 30 Katika upunguzaji wa maumivu, kazi ya mwanaonkolojia wa mnururisho ni kulinganisha utaratibu wa matibabu na hali ya kimatibabu ya mgonjwa, ilhali katika wagonjwa wanaoponywa, utaratibu wa matibabu hulinganishwa na hatua ya kimsingi ya uvimbe. Uingiliaji kati kwa wagonjwa ambao hawana matibabu ya saratani ambayo yana uwezekano mzuri wa kuitikia dawa haupendekezwi. Upasuaji, hali ya kuwekwa wazi kwa mnururisho au tibakemikali havipendekezwi kwa mgonjwa aliye katika hali isiyoweza kutibika. Katika upunguzaji wa maumivu, kazi ya mawanaonkolojia wa mnururisho ni kulinganisha utaratibu wa matibabu na hali ya kimatibabu ya mgonjwa, ilhali katika wagonjwa wanaoponywa, utaratibu wa matibabu hulinganishwa na hatua ya kimsingi ya uvimbe. Uingiliaji kati kwa wagonjwa ambao hawana matibabu ya saratani ambayo yana uwezekano mzuri wa kuitikia dawa haupendekezwi. Upasuaji, hali ya kuwekwa wazi kwa mnururisho au tibakemikali havipendekezwi kwa mgonjwa aliye katika hali isiyoweza kutibika.
32
Slaidi Hali mbili za jumla katika utunzaji wa kupunguza maumivu kwa saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea 31 Utunzaji wa kupunguza maumivu wa saratani ya mlango wa kizazi isiyodhibitiwa huzingatia hali mbili za kimsingi, ambazo husababisha matatizo yafuatayo ya kimatibabu: Kuibuka tena katika fupanyonga Maumivu ya fupanyonga Uvujaji wa damu Uzuiaji wa ndani ya vena Uzuiaji wa ureta Ugonjwa wa kimetastasisi Maumivu ya mifupa Mivunjiko ya kipatholojia Utunzaji wa kupunguza maumivu ya saratani ya mlango wa kizazi isiyodhibitiwa huzingatia hali mbili za kimsingi: kuibuka tena kwa ugonjwa kwenye fupanyonga na ugonjwa wa kimetastasisi.
33
32 Maumivu ya fupanyonga Slaidi
Kuwekewa mnururisho kwa mara kwa mara kwa uvimbe ulio kwenye fupanyonga kwa kutumia taratibu zinazoitwa hypofractionated regimens hutoa tulizo la haraka kwa maumivu ya fupanyonga. Utaratibu wa Hypofractionation: vipimo vya 20 Gy katika sehemu 5 (wiki moja) vipimo vya 30 Gy katika sehemu 10 (wiki mbili) vipimo vya 8 Gy katika sehemu moja Kuwekewa mnururisho kwa uvimbe katika fupanyonga kwa kutumia taratibu za hypofractionated regimens hutoa tulizo la haraka kwa maumivu ya fupanyonga
34
33 Uvujaji damu wa Jinakolojia Slaidi
Uvujaji damu kutoka katika jeraha lisilodhibitiwa katika mlango wa kizazi kwa kawaida hutokana na mchirizo wa veni kutoka kwenye uvimbe. Udhibiti unaweza kujumuisha: Kulazwa hospitalini au mapumziko ya kitandani Ufungaji wa uke Tibaredio ya upunguzaji wa maumivu: Kwa wagonjwa walio na matarajio ya muda mrefu zaidi wa kuishi: Utaalamu wa tibaredio wa kiwango cha kawaida yaani Fractionation: vipimo 40 Gy katika sehemu16 vipimo 50 Gy katika sehemu 25 Kwa wagonjwa walio katika hali mbaya kwa jumla /au matarajio ya muda mfupi zaidi wa kuishi: Utaalamu wa tibaredio wa kiwango cha chini yaani Hypofractionation: vipimo 20 Gy katika sehemu 5 vipimo 30 Gy katika sehemu 10 vipimo 8 Gy katika sehemu 1 Uvujaji wa damu kutoka kwenye jeraha lisilodhibitiwa katika mlango wa kizazi kwa kawaida huwa linatokana na mchirizo wa veni kutoka kwenye uvimbe. Udhibiti unaweza kuwa ni pamoja na: Kulazwa hospitalini au mapumziko ya kitandani, Ufungaji wa uke, Tibaredio ya kupunguza maumivu.
35
Uzuiaji katika veni 34 Slaidi Tibu maumivu
Hakikisha kuwa hakuna mvilio wa damu kwenye veni Hakikisha kuwa hakuna uzuiaji kwenye limfu kutokana na upasuaji wa fupanyonga na tibaredio ya baada ya upasuaji Inua kiundo Kuganda kwa kiasi kidogo ili kupunguza kuvimba Tibaredio kwenye bonge la fupanyonga Endapo kutakuwa na uzuiaji kwenye veni, fuata hatua zilizoelezwa katika slaidi hii.
36
35 Uzuiaji kwenye ureta Slaidi
Uzuiaji kwenye ureta ni jambo la kawaida mno kwa wagonjwa walio na saratani ya mlango wa kizazi isiyodhibitika. Vigezo vya uteuzi vinafaa kutumika kwa wagonjwa walio na saratani isiyotibika kabla ya kutumia utaratibu wa kufungua njia za figo uitwao percutaneous nephrostomy. Kwa wagonjwa wasio na chaguo lenye manufaa la kupunguza maumivu faida ya utaratibu huu ni ndogo mno. Tibaredio katika fupanyonga huenda ikafungua uzuiaji wa ureta. Uzuiaji kwenye ureta ni jambo la kawaida mno kwa wagonjwa walio na saratani ya mlango wa kizazi isiyodhibitika. Wagonjwa walio na saratani isiyotibika wanafaa kuchaghuliwa kwa umakini kabla ya kutumia utaratibu wa kufungua njia za figo uitwao percutaneous nephrostomy. Katika wagonjwa wasio na chaguo lenye manufaa la kupunguza maumivu faida ya utaratibu huu ni ndogo mno. Tibaredio katika fupanyonga huenda ikafungua uzuiaji wa ureta.
37
36 Mbinu ya tibaredio (1) Slaidi
Nyuga halisia za mbele na nyuma na za upande zinazolengwa katika mnururisho wa fupanyonga katika saratani ya mlango wa kizazi kwa kutumia mbinu iitwayo 4-field “box” technique Slaidi hii inaonyesha nyuga halisia za mbele na nyuma na za upande zinazolengwa katika mnururisho wa fupanyonga katika saratani ya mlango ya kizazi kwa kutumia mbinu iitwayo 4-field “box” technique.
38
37 Mbinu ya tibaredio (2) Slaidi
Ugavi wa kipimo cha dawa ya mnururisho katika fupanyonga kwa kutumia mbinu ya 4-field “box”: Ncha ya katikati ndiyo inayotumika kwa uwekaji wa dawa na ndipo panarejelewa. Eneo lilowekwa mistari hupokea zaidi ya asilimia 95 ya kipimo cha dawa kilichopendekezwa (kutoka kwa Ripoti ya 50 ya ICRU) Slaidi hii inaonyesha kipimo cha dawa cha mnururisho kilichogawanywa kwenye fupanyonga kwa kutumia mbinu ya 4-field “box” technique.
39
38 Metastasisi ya maumivu ya mifupa Slaidi
Matokeo ya utulizaji wa maumivu yanayotokana na mnururisho katika metastasisi ya maumivu ya mifupa yametambulika kwa miaka mingi. Tibaredio ya kulenga ndiyo pengine matibabu yanayofaa zaidi kwa maumivu ya mfupa yanayopatikana katika eneo maalum: Maumivu ya mifupa yaliyo mahali maalum: Sehemu moja ya 8 Gy (matibabu mapya kwa kipimo cha dawa cha pili cha 8 Gy huenda yakahitajika katika asilimia ya wagonjwa). Hakuna jukumu la matibabu ya vipimo mbalimbali katika metastasisi ya mfupa isiyokuwa ngumu Maumivu ya sehemu mbalimbali yanayotokana na metastasisi ya mifupa isiyo changamani: Toa tibaredio ya kulenga mahali maalum kutoka nje kwelekea sehemu iliyo na maumivu zaidi Rejelea tiba aina ya radionuclide kwa kutumia: Strontium-89 au Rhenium-186 iwapo maumivu ya mfupa yanatokana na metastasisi ya seli za mfupa (osteoblastic bone metastasis) Matokeo ya utulizaji wa maumivu yanayotokana na mnururisho katika metastasisi ya maumivu ya mifupa yametambulika kwa miaka mingi. Tibaredio ya kulenga ndiyo pengine matibabu yanayofaa zaidi kwa maumivu ya mfupa yanayopatikana katika eneo maalum.
40
39 Mivunjiko ya kipatholojia Slaidi Zuia kusonga Tibu maumivu
Dhukuru upasuajiwa ndani wa kuimarisha (kulingana na hali ya jumla na matarajio ya muda wa kuishi ya mgonjwa) Tibaredio iliyoelekezwa kutoka nje kwenye jeraha Ikiwa mgonjwa hawezi kufanyiwa upasuaji: tibaredio ya upunguzaji wa maumivu na uzuiaji wa nje wa kusonga. Ikiwa kuna mivunjiko ya kipatholojia, fuata hatua zilizoelezewa kwenye slaidi hii.
41
40 Tibakemikali ya upunguzaji wa maumivu Slaidi
Katika kasinoma ya mlango wa kizazi iliyoendelea, inayorudi au iliyo na metastasisi, mseto wa tibakemikali ulio na cisplatin unaweza kusababisha kima cha mwitikio cha asilimia (upunguzaji wa uvimbe na kuboresha hali ya dalili. Visababishi amilifu vya tibakemikali katika hali hii ni: Cisplatin Ifosfamide Paclitaxel Topotecan Katika kasinoma ya mlango wa kizazi iliyoendelea, inayorudi au iliyo na metastasisi , mseto wa tibakemikali ulio na cisplatin unaweza kusababisha kima cha mwitikio cha asilimia (upunguzaji wa uvimbe na kuboresha kwa hali ya dalili)
42
Slaidi 41 4. Matibabu ya dalili za kawaida katika saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea
43
Slaidi Utunzaji wa nyumbani wa kupunguza maumivu na matibabu ya dalili za kawaida 42 Utunzaji wa kupunguza maumivu unaweza kufanywa nyumbani. Matatizo yanaweza kudhibitiwa nyumbani huenda yakajumuisha: Kutokwa na umajimaji kwenye uke Kutokwa na damu kwenye uke Nasuri Kichefuchefu na kutapika Kuendesha au uyabisi wa tumbo Homa Kupoteza hamu ya kula, uchovu, unyonge, kudhoofika Uvimbe kwenye mguu Vidonda vya kitandani Kutwetatweta Mfadhaiko Utunzaji wa kupunguza maumivu unaweza kufanywa nyumbani. Slaidi hii inatoa muhtasari wa baadhi ya matatizo ambayo yanaweza kudhibitiwa nyumbani.
44
43 Kutokwa na umajimaji na/au damu kwenye uke Slaidi
Huenda hizi huenda zikawa ishara za kwanza za saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea Kutokwa damu huwa mara nyingi ni kwa kiwango kidogo lakini huenda kukazildi Tafuta ishara za maambukizi/uwepo wa vidonda Matibabu yatategemea hali huenda – tibakemikali ya kupunguza maumivu huenda ikapendekezwa kwa visa teule Ufungaji na/au kuongezewa damu huenda vikapendekezwa pia katika visa vya hali mbaya zaidi Komesha matumizi ya dawa zozote (yaani ibuprofen ) ambazo huenda zinazosababisha / zidisha uvujaji damu Maambukizi yanaweza kutibiwa kwa madawa aina ya viua vijasumu (antibiotics) na/au viua kuvu (antifungals) kulingana na chanzo Huenda kutokwa na umajimaji na/au damu kwenye uke zikawa ishara za kwanza za saratani ya mlango wa kizazi iliyoendelea. Kutokwa damu huwa mara nyingi ni kwa kiwango kidogo lakini huenda kukazildi. Maambukizi yanaweza kutibiwa kwa kutumia viua vijasumu na/ au viua kuvu kulingana na chanzo.
45
44 Kichefuchefu na kutapika Slaidi
Hutokea mara nyingi katika siku chache za kwanza baada ya kuanza kutumia opioidi Zingatia kila mara sababu nyinginezo za kusababisha kichefuchefu na kutapika yaani uzuiaji wa uchengelele, dawa nyinginezo, kudhoofika kwa figo Kutumia dawa aina ya Metoclopramide (miligramu 10 kwa kinywa / chini ya ngozi/ndani ya mshipa kwa kila saa 4-6) ndilo chaguo la kwanza katika hali nyingi. Hata hivyo, usitumie katika visa vya uzuiaji kamili wa uchengelele Ikiwa kuna uzuiaji wa uchengelele, tumia dawa ya Haloperidol (miligramu chini ya ngozi/ndani ya mshipa kwa kila saa 6-12) badala yake Fuatilia ikiwa kutaibuka athari za kiakili (extra-pyramidal) wakati wa matumizi ya dawa hizi mbili Kichefuchefu na kutapika hutokea mara nyingi katika siku chache za kwanza baada ya kuanza kutumia opioidi. Sababu nyinginezo za kusababisha kichefuchefu na kutapika (kama vile uzuiaji wa uchengelele, dawa nyinginezo, kudhoofika kwa figo) zinafaa kuzingatiwa kila mara.
46
45 Uyabisi wa tumbo Slaidi Uzuiaji wa uyabisi wa tumbo ni muhimu sana
Uyabisi wa tumbo ni jambo la kawaida sana baada ya kuanza kutumia opioidi endapo halikutarajiwa na kuzuiliwa. Fanya hivyo kwa kuanza kutumia haluli pindi matumizi ya opioidi yanapoanza Anza kwa kutumia dawa aina ya peristaltic, yaani Bisacodyl (miligramu 5-15 kwa kinywa mara mbili kwa siku) au Senna (tembe mbili kwa kinywa wakati wa kulala) na ongeza ikihitajika Madawa ya ziada (lactulose au sorbitol), utaratibu wa kuingiza madawa aina ya suppositories au enema huenda ukahitajika Pia ikiwa inawezekana mfanye mgonjwa aongeze unywaji wake wa viowevu Ondoa sababu nyinginezo za uyabisi wa tumbo, yaani dawa nyinginezo, upungufu wa maji mwilini, uzuiaji wa uchengelele,… Uzuiaji wa uyabisi wa tumbo ni muhimu sana. Uyabisi wa tumbo ni jambo la kawaida sana baada ya kuanza kutumia opioidi endapo halikutarajiwa na kuzuiliwa. Fanya hivyo kwa kuanza kutumia haluli pindi matumizi ya opioidi yanapoanza. Pia ikiwa inawezekana mfanye mgonjwa aongeze unywaji wake wa viowevu. Hakikisha kila mara kuwa umeondoa sababu nyinginezo za uyabisi wa tumbo, kama vile dawa nyinginezo, upungufu wa maji mwilini, uzuiaji wa uchengelele.
47
46 Mfadhaiko Slaidi Maumivu mara nyingi huambatana na mfadhaiko
Chaguo za matibabu hujumuisha dawa zinazokabiliana na wasiwasi na mfadhaiko (anxiolytics na antidepressants), msaada wa ushauri nasaha, ushauri wa kiroho, na msaada wa familia Marejeleo kwa mtaalamu wa magonjwa ya akili yanapendekezwa iwapo yanapatikana, hasa pale ambapo matibabu ya dawa dhidi ya mfadhaiko zinahusika Maumivu mara nyingi huambatana na mfadhaiko. Chaguo za matibabu hujumuisha dawa zinazokabiliana na wasiwasi na mfadhaiko (anxiolytics na antidepressants), msaada wa ushauri nasaha, ushauri wa kiroho, na msaada wa familia. Marejeleo kwa mtaalamu wa magonjwa ya akili yanapendekezwa iwapo yanapatikana, hasa pale ambapo matibabu ya dawa dhidi ya mfadhaiko zinahusika.
48
5. Dawa zinazotumika zaidi
Slaidi 47 5. Dawa zinazotumika zaidi
49
48 Paracetamol Slaidi Hali za matumizi: maumivu ya kiwango kidogo
Kipimo: miligramu kwa kinywa kila baada ya saa nne. Kipimo cha juu zaidi gramu 4/siku Hali ambazo dawa hizi hazifai kamwe kutumika: kudhoofika kwa ini au figo, jihadhari ikiwa unatumia dawa za kuzuia damu kuganda Paracetamol inapendekezwa kwa maumivu ya kiwango kidogo.
50
49 Ibuprofen Slaidi Hali za matumizi: maumivu ya kiwango kidogo
Kipimo: miligramu kwa kinywa kila baada ya saa 6 Hali ambazo dawa hizi hazifai kamwe kutumika: vidonda vya tumboni, kudhoofika kwa figo au idadi ndogo ya i kwa puru au idadi ya chini ya seli aina ya platelet, mzio unaopita kiasi kwa matumizi ya aspirin au dawa nyinginezo za kuzuia kuvimba ambazo si steroidi yaani aina non-steroidal anti-inflammatory (NSAIDs) Tahadhari: -Kichefuchefu, kutapika, na maumivu ya tumboni ni baadhi ya athari - Inaweza pia kusababisha kutokwa na damu, kusita kwa moyo, shinikizo la damu, na hypertension na kutatizika kwa mfumo wa figo Ibuprofen hupendekezwa vilevile kwa maumivu ya kiwango kidogo.
51
50 Amitriptyline Slaidi Hali za matumizi: maumivu ya neva au mfadhaiko
Kipimo: miligramu kwa kinywa wakati wa kulala, huku kikiongezwa polepole hadi gramu 150 ikiwa inahitajika Hali ambazo dawa hizi hazifai kamwe kutumika: mshtuko wa moyo katika siku za punde, mpigo wa papo usio wa kawaida (arrhythmias), kudhoofika kwa kiwango cha juu sana kwa ini Tahadhari: inaweza kusababisha mpozo, uyabisi wa tumbo, kukauka kwa kinya, kiwi cha macho, kufunga mkojo Amitriptyline hupendekezwa kwa maumivu ya neva na mfadhaiko.
52
Slaidi Gabapentin 51 Hali ya matumizi: maumivu ya kineuropathia (neuropathic). Athari chache zaidi kuliko amitriptyline Kipimo: anza kwa kipimo cha chini cha miligramu 100 kwa kinywa mara tatu kwa siku na ongeza vipimo katika vipindi vya siku 3-5 hadi miligramu kwa kinywa mara tatu kwa siku Tahadhari: huenda ikasababisha usingizi, kizunguzungu, kuvimba kwa viungo vya chini, kutetemeka; rekebisha kipimo katika hali ya kutatizika kwa mfumo wa figo. Gabapentin hupendekezwa kwa maumivu ya kineuropathia, na ina athari chache zaidi kuliko amitriptyline.
53
Slaidi Steroidi 52 Hali ya matumizi: mbalimbali ukiwemo mfinyo wa uti wa mgongo , mfinyo wa neva, maumivu ya mifupa , uzuiaji wa kudhuru wa uchengelele, kichefuchefu, kukosa hamu ya chakula, kutwetatweta Kipimo: miligramu 4-8 kwa kinywa/chini ya ngozi/dani ya mshipa mara moja kwa siku Tahadhari: huenda ikaongeza kiwango cha sukari kwenye damu, kusababisha fadhaa na ukosefu wa usingizi, kuongeza hatari ya kuwa na vidonda kwenye tumbo au utumbo ikiwa inatumika pamoja na dawa aina za NSAID, ongezeko la uwezekano wa maambukizi. Kukomesha matumizi kwa ghafla kunaweza kuhimiza kiwewe cha tezi za adrena (adrenal crisis). Hali ambazo dawa hizi hazifai kamwe kutumika: ugonjwa wa kisukari aina ya 1 (diabetes mellitus) ambao hujadhibitiwa Steroidi zinapendekezwa kwa matatizo mbalimbali ukiwemo mfinyo wa uti wa mgongo , mfinyo wa neva, maumivu ya mifupa , uzuiaji wa kudhuru wa uchengelele, kichefuchefu, kukosa hamu ya ch.akula. kutwetatweta
54
53 Dihydrocodeine na Codeine Slaidi
Hali ya matumizi: maumivu ya kiwango cha chini hadi cha wastani. Kipimo: Codeine: miligramu kwa kinywa kila baada ya saa 4 Dihydrocodeine: miligramu15-30 kwa kinywa kila baada ya saa 4 Hali ambazo dawa hizi hazifai kamwe kutumika: Mzio wa kweli kwa opioidi, ambao ni nadra sana Udhaifu wa figo Mbali na hizi, hakuna hali ambazo dawa hizi hazifai kutumika ikiwa zitatayarishwa ipasavyo Tahadhari: - Mara nyingi husababisha uyabisi wa tumbo hivyo wanawake wanafaa pia kutumia haluli, na kunywa viowevu vingi sana Huenda pia ikasababisha usingizi, kichefuchefu, kutapika, kuwashwa na kuchanganyikiwa Kwa nadra inaweza kusababisha matatizo ya mfumo wa kupumua Dihydrocodeine na codeine hupendekezea kwa maumivu ya kiwango cha chini hadi cha wastani
55
Slaidi Mofini 54 Hali ya matumizi : maumivu ya wastani hadi maumivu makali Kipimo: Anza kwa miligramu 10 kwa kinywa baada ya kila saa 4. Ongeza inavyohitajika ili kudhibiti maumivu kwa kipindi cha saa 4. Hali ambazo dawa hizi hazifai kamwe kutumika: mzio wa kweli kwa opioidi, ambao ni nadra sana ugonjwa mkali wa mfumo wa kupumua, udhaifu wa figo mbali na hizi, hakuna hali ambazo dawa hizi hazifai kutumika ikiwa zitatayarishwa ipasavyo Tahadhari: - Mara nyingi husababisha uyabisi wa tumbo hivyo wanawake wanafaa pia kutumia haluli, na kunywa viowevu vingi sana Huenda pia ikasababisha usingizi, kichefuchefu, kutapika, kuwashwa na kuchanganyikiwa Kupumua kwa kina kifupi sana, mzubao, kuzimia kwa muda mrefu (coma), au kutoweza kabisa kupumua ni baadhi ya ishara za kuzidisha kipimo Mofini inapendekezwa kwa maumivu ya wastani hadi maumivu makali.
56
55 Kumbusho kuhusu opioidi (mofini na kodeini) Slaidi
Pindi mwanamke aliye na saratani iliyoendelea anapoanza kutumia opioidi, kwa kawaida atahitaji kuendelea kuzitumia kwa udhibiti wa maumivu katika maisha yake yote yanayosalia. Kutawaliwa (addiction) kwa mgonjwa aliye na maradhi yasiyotibika si jambo la kuzingatia Uongezaji wa kipimo wa mara kwa mara unahitajika ili kuendelea kudhibiti maumivu Kodeini ni ghali sana katika nchi nyingi zenye rasilimali ya chini na ina imetiliwa mipaka ya kiwango kwa hivyo wagonjwa wengi huhitajika kuhamia kwenye mofini, ambayo ni ya bei nafuu zaidi Uoga wa kutawaliwa na dawa mara nyingi ni kizuizi cha kuweza kufikiamatumizi ya opioidi kwa wagonjwa wa saratani. Inafaa kusisitizwa kwamba kutawaliwa kwa mgonjwa aliye na maradhi yasiyotibika SI swala la kuzingatia. Kumbuka kwamba kodeini ni ghali sana katika nchi nyingi zenye rasilimali ya chini na ina imetiliwa mipaka ya kiwango kwa hivyo wagonjwa wengi huhitajika kuhamia kwenye mofini, ambayo ni ya bei nafuu zaidi. Matumizi ya kodeini hayahimizwi Barani Afrika kwa sasa, ila tu kama mofini ya kunywewa haipatikani.
57
56 Vizuizi vya kufikia tulizo la maumivu Slaidi
Kila mwaka wagonjwa milioni 5.5 waliougua saratani isiyoweza kutibika, wanaoishi katika nchi zilizo na mfiko wa dawa zinazodhibitiwa wa kiwango cha chini au usiokuwepo kabisa, huteseka bila ya matibabu ya kutosha (makadirio ya WHO) Nchi zenye mapato ya juu huchukua karibu asilimia 91 ya mofini inayotumiwa ulimwenguni ingawa nchi hizi hujumuisha asilimia 17 pekee ya idadi nzima ya watu. Katika nchi zenye mapato ya chini na ya wastani (asilimia 83 ya idadi ya watu duniani) asilimia 9 ya jumla ya mofini hutumiwa (Kamati ya Kimataifa ya Udhibiti wa Nakotiki, 2008) (International Narcots Control Board, 2008) Mojawapo ya vizuizi vya mfiko wa tulizo la maumivu la kufaa kwa watu wote ni kuwa serikali na makundi ya kimataifa mara nyingi huzingatia upande wa udhibiti wa dawa za kulevya (narcotics) na kupuuza jukumu lao la kuhakikisha mfiko wa vituliza maumivu vya opioidi kwa madhumuni ya kimatibabu Shirika la Afya Duniani linakadiria kuwa kila mwaka wagonjwa milioni 5.5 waliougua saratani isiyoweza kutibika, wanaoishi katika nchi zilizo na mfiko wa dawa zinazodhibitiwa wa kiwango cha chini au usiokuwepo kabisa, huteseka bila matibabu ya kutosha. Marejeleo ya takwimu za 2008 za Kamati ya Kimataifa ya Udhibiti wa Nakotiki (International Narcotics Control Board ) kuhusu matumizi ya mofini zilizoripotiwa na serikali yanaonyesha kuwa nchi zenye mapato ya juu huchukua karibu asilimia 91 ya mofini inayotumiwa ulimwenguni ingawa nchi hizi hujumuisha asilimia 17 pekee ya idadi nzima ya watu. Katika nchi zenye mapato ya chini na ya wastani (asilimia 83 ya idadi ya watu duniani) asilimia 9 ya jumla ya mofini hutumiwa . Mojawapo ya vizuizi vya mfiko wa tulizo la maumivu la kufaa kwa watu wote ni kuwa serikali na makundi ya kimataifa mara nyingi huzingatia upande wa udhibiti wa dawa za kulevya (narcotics) na kupuuza jukumu lao la kuhakikisha mfiko wa vituliza maumivu vya opioidi kwa madhumuni ya kimatibabu
58
Slaidi Kufanya vituliza maumivu vya opioidi kupatikana kwa urahisi pale vinavyohitajika 57 Maumivu ya saratani yanaweza kutibiwa kwa usalama na kwa ufanisi kwa kutumia vituliza maumivu kya opioidi, kama vile mofini. Wanafamasia wanaweza kutayarisha kwa urahisi mmumunyo wa kunyweka wa mofini kutoka kwenye poda, kwa gharama ya chini sana. Hapa tunaona mofini ya kunywewa ikiwa inamezwa na mgonjwa katika nyumba yake mwenyewe nchini Uganda, akiwa amezungukwa na timu ya utunzaji wa kupunguza maumivu. Baada ya maelekezo na maonyesho rahisi , mgonjwa ataweza kuutumia mmumunyo mwenyewe katika vipindi vya mara kwa mara ili maumivu yake yasiwahi kurudi. Chupa ya kawaida ya mofini ya kijani (miligramu 5 kwa kila mililita) itaweza kumchukua mgonjwa wa wastani kwa siku 10 za vipimo vya kuleta nafuu na inaweza kutayarishwa kwa gharama ya mkate. Picha kwa hisani ya: Hifadhi za nyaraka za Hospisi ya Uganda (kushoto); Dr Mhoira Leng, Cairdas (kulia)
59
58 Wakati wa kumhamisha mgonjwa hadi kwenye mazingira ya hospitali
Slaidi Wakati wa kumhamisha mgonjwa hadi kwenye mazingira ya hospitali 58 Mgonjwa (kama anayo fahamu) na jamii yake ya karibu wanafaa kuhusishwa katika uamuzi wa kumhamisha hadi hospitalini Ikiwa mgonjwa anaaga dunia, hafai kuhamishwa katika dakika ya mwisho Wakati mwafaka wa kumhamisha mgonjwa: Uvujaji mkali wa damu kwenye uke Upungufu mkali wa maji mwilini au kuendesha kwa zaidi ya saa 48 Kichefuchefu na kutapika kubaya sana Damu kwenye kinyesi Homa ya digri za sentigredi 39 kwa zaidi ya saa 48 Mtukutiko wa maungo (degedege) Kuchanganyikiwa Maumivu makali kwenye tumbo Maumivu makali yasiyodhibitika na opioidi Vidonda kadhaa vya kitandani vulivyo ingiwa vidudu Matatizo makali ya kupumua Majaribio ya kujiua Utunzaji wa kufanyiwa nnyumbani una mipaka yake. Slaidi hii inatoa muhtasarii wa nyakati ambazo mgonjwa anafaa kuhamishwa hadi katika mazingira ya hospitali
60
59 Utunzaji wa mwisho wa maisha Slaidi
Tambua kwamba asili zote zilizosababisha hali hii zinazoweza kurekebishwa zimeshatiliwa maanani Lengo ni kutunza na kufariji wakati wa siku na saa za mwisho za maisha Matumizi ya matibabu na dawa yasiyohitajika kwa lazima yanafaa kukatizwa (tibaredio, tibakemikali, kuongezewa damu, viua vijasumu, taratibu za kuingilia) Mawasiliano na familia ya pamoja na watoa huduma yanafaa kuendelezwa na kuhimizwa Zingatia udhibiti wa maumivu Tibu matatozi kama yale ya: fadhaa, utemaji wa mfumo wa upumuaji, kichefuchefu na kutapika, kutwetatweta Mahitaji ya kiroho na kidini yanafaa kushugulikiwa. Wakati wa utunzaji wa mwisho wamaisha, lengo ni kutunza na kufariji, kuzingatia udhibiti wa maumivu, mawasiliano na mgonjwa na jamii na kushughulikia mahitaji ya kiroho na kidini.
61
60 Marejeo na nyenzo muhimu Slaidi
Palliative Medicine. Pain and symptom control in the cancer and/or AIDS patient in Uganda and other African countries, Hospice Africa Uganda 2002, kinapatikana kwa Kiingereza na Kifaransa INCTR Palliative Care Handbook, 2008 Palliative Care Toolkit, Worldwide Palliative Care Alliance/Help the Hospices, 2008 Medical Care of the Dying, Victoria Hospice Society 4th Edition, 2006 Fraser Health Hospice Palliative Care Symptom Guidelines, 2009 PCF3 Palliative Care Formulary, 3rd Edition, 2007 Comprehensive Cervical Cancer Control. A guide to essential practice. WHO, Geneva, 2006 Criteria for Palliation of Bone Metastases - Clinical Applications, IAEA-TECDOC-1549, 2007, available in English, French and Spanish The Role of Radiotherapy in the Management of Cancer Patients infected by the Human Immunodeficiency Virus (HIV), IAEA-TECDOC-1224, 2001 Improving Cancer Care. Increased Need for Radiotherapy in Developing Countries, IAEA Bulletin, 43/2/2001 The Applied Sciences of Oncology (ASO) Distance Learning Course in Radiation Oncology for Cancer Treatment (Updated Version of the ASO Distance Learning Course), IAEA, Vienna, 2010 IAEA Syllabus for the Education and Training of Radiation Oncologists, IAEA Training Course Series No. 36 (IAEA-TCS-36), IAEA in Vienna, Austria, 2009 International Palliative Care Resource Center, GAPRI – Global Access to Pain Relief Initiative,
62
Asante 61 Wasilisho hili linapatikana katika: www.uicc.org/curriculum
Slaidi 61 Asante Wasilisho hili linapatikana katika: Asante kwa usikivu wenu. Wasilisho hili linaweza kupakuliwa katika tovuti ya UICC.
Similar presentations
© 2025 SlidePlayer.com Inc.
All rights reserved.